Print this Page

Tangazo kwa Watanzania

Ubalozi unawatangazia Watanzania wote wenye uraia wa Tanzania kuwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanzisha utaratibu wa kutoa huduma kwa haraka “fast track” ya utambuzi na usajiri kwa watakaokwenda nyumbani.

Ili kufanikisha zoezi hilo, Mamlaka imemteua Bi Rose Mdami kuwa Afisa Dawati atakayeshughulikia masuala ya Diaspora ndani ya Mamlaka ya NIDA. Dawati hilo litakuwa katika jengo la Magereza lililopo Barabara ya Kivukoni, jijini Dar es salaam.

Kutokana na changamoto zinazokabili mamlaka hiyo, kwa sasa NIDA haitoweza kufanya zoezi la utambuzi na usajiri nje ya nchi. Tunaomba wananchi hao kufika ofisi ya NIDA ili kupata huduma ya “fast track” pindi watakapokuwa Tanzania.

Permanent link to this article: http://tanzaniahighcomm.co.uk/?page_id=647