Print this Page

Utaratibu wa kupata pasipoti mpya

KUNUNUA FOMU

Mwombaji anaweza kuja Ubalozini na pasipoti aliyonayo ili kununua fomu au atume “Pound 5”,- (malipo ya fomu kwa “Postal Order”). Aidha, alete bahasha yenye anuani yake iliyobandikwa stampu za rejista ili apelekewe fomu.

 

ALAMA ZA VIDOLE NA TAHADHARI

 1. Katika utoaji wa pasipoti mpya lazima mwombaji achukuliwe alama za vidole (`finger prints’) na kuweka sahihi kwa mkono wake mwenyewe mbele ya afisa mhusika. Hivyo, tarehe ya kuchukuliwa alama za vidole; mwombaji apige simu(mida mizuri ya kupiga simu kati ya saa 3:30-5:00) au e-mail.
 2. Mwombaji LAZIMA aje UBALOZINI ili kutia sahihi fomu na kuchukuliwa alama za vidole.
 3. Pasipoti mpya zitatolewa Makao Makuu ya Uhamiaji, Dar es Salaam na zitaletwa Ubalozini kwa mfuko maalum.
 4. Ubalozi utatuma pasipoti mpya kwa mwombaji kwa kutumia bahasha iliyoandikwa anuani na mwombaji na kuwekwa stampu za rejista. Pasipoti ya zamani itabidi iwe ´cancelled’ ili nayo irudishwe kwa Mwombaji katika bahasha moja na pasipoti mpya. Hivyo, mawasiliano na Ubalozi ni muhimu kwani pasipoti mpya haitatolewa kabla ya zamani kuwa `cancelled’.

*NB:

Watanzania wanaokwenda nyumbani siku za karibuni wanashauriwa na wanaruhusiwa kuomba pasipoti mpya wakati wakiwa nyumbani katika ofisi za uhamiaji Tanzania. Kufanya hivyo kutawaharakishia kupata pasipoti hizo. Kwa wale ambao pasipoti zao zipo chini ya miezi sita watatakiwa kuomba “Emergenc Travel Document” Ubalozini.

 A. Mahitaji:

 • Fomu ya pasipoti (CT 5) iliyojazwa kikamilifu kwenye vipengele vyote.
 • Picha tano (5) za pasipoti zenye “background” ya rangi ya “blue” au rangi ya maji ya bahari. (Ziwe za hivi karibuni).
 • Kivuli cha pasipoti ya zamani ukurasa 1 na ukurasa wenye picha na taarifa muhimu za muombaji (bio-data page).
 • Kivuli cha kibali cha makazi au Visa.
 • Kivuli cha cheti cha kuzaliwa/kiapo cha kuzaliwa cha mwombaji.
 • Kivuli cha cheti cha kuandikisha uraia wa Tanzania wa mwombaji.
 • Deed Poll ya badiliko la majina kwa wanaotaka kubadili jina.
 • Kivuli cha cheti cha ndoa kwa wanaotaka kubadilisha jina kwa sababu ya ndoa.

 

Kama pasipoti imepotea au kuibiwa ni lalzima kuleta

 • “Lost report” (www.immobilise.com).
 • Maelezo binafsi kwa maandishi kueleza yafuatayo:
 • Taarifa za pasipoti iliyopotea kwa maana ya Namba ya pasipoti, tarehe na mwaka ilipotolewa na DN yako;
 • Mazingira ya kupotea/kuibiwa kwa pasipoti; na
 • Mahali na tarehe ya kupotea/kuibiwa kwake.
 • Tangazo la gazeti kuhusu kupotea/kuibiwa kwa pasipoti hiyo.
 • Cheti cha kuzaliwa

 

FOMU IJAZWE KWA HERUFI KUBWA

 1. a) Wakati wa kujaza fomu `Section 2′ tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa wazazi ni LAZIMA. Hata wazazi waliofariki.
 2. b) Kama kuna sababu ya kubadilisha jina lazima hati husika za sababu ya kubadili jina ziletwe – k.m. cheti cha ndoa.
 3. d) Acha au usijaze kipengele cha sita (6) katika fomu kwa kuzingatia Maelezo Muhimu kwenye kipengele cha pili (2) – waliotajwa hawapatikani nje ya Tanzania.
 4. e) Kila fomu ina namba moja haitumiki kwa watu wawili. Mwombaji asithubutu kutoa nakala (photocopy) ili itumike kwa mwombaji mwingine.
 5. Inatahadharishwa kuwa fomu za uombaji pasipoti zilizokosewa au kufutwafutwa hazitakubalika itabidi mwombaji anunue fomu nyingine. Ni vema kabla ya kujaza fomu mwombaji atoe nakala (photocopy) ya fomu aijaze kwanza kila kipengele ili baadaye anakili katika fomu aliyopelekewa kuepuka makosa, kufutwafutwa na kununua fomu nyingine.

Permanent link to this article: http://tanzaniahighcomm.co.uk/?page_id=556